• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Burundi lautaka Umoja wa Ulaya kuondoa vikwazo dhidi ya nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2017-05-11 09:51:48
     

    Mabaraza ya bunge la Burundi yameuandikia barua Umoja wa Ulaya kutaka umoja huo uiondolee vikwazo Burundi.

    Barua hiyo imeandikwa wakati mkutano utakaoshirikisha nchi za Umoja wa Ulaya na nchi za kundi la Afrika, Caribbean na Pasifiki ACP ukitarajiwa kufanyika Juni 19 hadi 21 mwaka huu.

    Barua hiyo imesema, Burundi sasa imekuwa nchi yenye amani, hali imeboreshwa tangu mwezi Aprili mwaka 2005 lilipotokea jaribio la mapinduzi.

    Kwa mujibu wa bunge la nchi hiyo, hali ya haki za binadamu pia imeboreshwa. Wahalifu zaidi ya elfu 10 wamepelekwa mahakamani, na wafungwa elfu 2.5 wameachiwa huru kutokana na msamaha wa rais mwanzoni mwa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako