• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KQ kuzindua safari ya moja kwa moja kwenda Marekani mwakani

    (GMT+08:00) 2017-05-11 09:52:08

    Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya anga Kenya KCAA Bw. Gilbert Kibe amesema, shirika la ndege la Kenya Kenya Airways (KQ) litazindua safari za moja kwa moja kwenda Marekani mwezi wa Aprili mwaka kesho.

    Bw. Kibe amesema, shirika hilo limepiga hatua kubwa katika kupata kibali cha kuzindua safari ya ndege kwenda Marekani.

    Pia amesema, shirika la ndege la Kenya limetoa ombi kwa wizara ya uchukuzi ya Marekani kupata idhini ya huduma ya usafiri wa ndege ili kuzindua safari ya moja kwa moja kwenda nchi hiyo.

    Amekadiria kuwa mchakato wa kupata idhini hiyo, huenda utachukua zaidi ya miezi 8.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako