• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China azungumza na mwenzake wa Korea Kuisni kwa njia ya simu

    (GMT+08:00) 2017-05-11 16:00:13

    Rais Xi Jinping wa China leo amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na rais mpya wa Korea Kusini Moon Jae-in.

    Rais Xi amempongeza Moon kwa ushindi wake kwenye uchaguzi wa rais nchini Korea Kusini, na kusema China na Korea Kusini ni majirani wa karibu na nchi muhimu katika eneo la Asia Mashariki. Amesema tangu nchi hizo zianzishe uhusiano wa kibalozi miaka 25 iliyopita, uhusiano wao umepata mafanikio mengi ambayo yanastahili kupongezwa. Ameeleza matumaini yake kwa serikali mpya ya Korea Kusini kuangalia kwa makini ufuatiliaji mkuu wa China, na kuchukua hatua za kivitendo kuhakikisha maendeleo tulivu na mazuri ya uhusiano wa pande hizo mbili.

    Kwa upande wake, rais Moon Jae-in amesema anaelewa ufuatiliaji mkubwa wa China, na serikali yake itajitahidi kuwasiliana na upande wa China, ili kushughulikia kwa mwafaka tatizo linalozikabili nchi hizo kwa sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako