• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yahoji uchunguzi unaofanywa na Marekani kuhusu uagizaji wa bidhaa za chuma

    (GMT+08:00) 2017-05-11 17:47:09

    Wizara ya Biashara ya China imehoji uchunguzi wa kibiashara unaofanywa na Marekani dhidi ya uagizaji wa bidhaa za chuma kutoka nchi sita ikiwemo China, na kusema hatua hiyo imepita kiasi.

    Katika tovuti ya wizara hiyo, mkuu wa mamlaka ya kurekebisha na kuchunguza biashara Wang Hejun ameeleza wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa vitendo vya kujilinda kibiashara kutoka kwa nchi hiyo kubwa kiuchumi duniani. Amesema Marekani inapaswa kushughulikia suala hilo kwa makini na kwa njia ya haki, na kujenga mazingira tulivu na ya kuaminika kwa ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya chuma.

    Wizara ya biashara ya Marekani imeamua kuanzisha uchunguzi dhidi ya uuzaji kwa bei ya chini zaidi wa mabaki ya vyuma vinavyotoka China, Ujerumani, Italia, Korea Kusini na Uswisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako