• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaikabidhi serikali ya mkoa wa Puntland nchini Somalia watuhumiwa watatu wa uharamia

  (GMT+08:00) 2017-05-11 20:49:55

  Wizara ya ulinzi ya China imethibitisha kuwa China imeikabidhi serikali ya mkoa wa Puntland nchini Somalia watuhumiwa watatu wa uharamia.

  Idara ya habari ya wizara hiyo imefahamisha kuwa tarehe 9 Aprili manowari ya Yulin ya jeshi la maji la China ilifanikiwa kuiokoa meli ya mizigo ya Tuvalu iliyotekwa nyara na maharamia na kuwakamata watuhumiwa watatu. Kwa mujibu wa sheria husika na mazeozi ya kimataifa, ijumaa iliyopita China iliwakabidhi watuhumiwa hao kwa serikali ya mkoa wa Puntland baada ya kufanya mawasiliano na serikali ya Somalia.

  Wizara hiyo imesema jeshi la China litaendelea kutuma manowari za kijeshi na kutekeleza jukumu la kulinda usalama wa meli zinazopita kwenye eneo la bahari ya Somalia, kutoa mchango mkubwa zaidi katika kulinda amani na utulivu wa kikanda, na kuhakikisha usalama wa njia muhimu za kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako