• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: URA yakusanya trilioni 10.5 ndani ya miezi 10

    (GMT+08:00) 2017-05-11 18:49:19

    Mamlaka ya kukusanya ushuru nchini Uganda URA imekusanya shilingi trilioni 10.5 ndani ya miezi 10 na inatarajia kukusanya zingine trilioni 2.9 kabla ya kukamilika kwa mwaka wa fedha.

    Hayo ni kwa mujibu wa Kamishena mkuu wa mamlaka hiyo Doris Akol wakati akizindua kamati ya kusajili mawakala wa kukusanya ushuru (TARC)

    Alisema majukumu ya kamati hiyo ni kutoa leseni kwa mawakala wote wanaoruhusiwa kukusanya ushuru kwa niaba ya URA.

    Kamati hiyo itakuwa na jukumu la kuweka viwango vinavyohitajika kwa mawakala na kutoa leseni.

    Bwana Henry Saaka, ambaye ni kamishena anayeshughulikia ushuru wa ndani ya nchi amesema baadhi ya mawakala hawafahamu biashara za wateja wao na mara nyingi wanawatoza pesa nyingi au kidogo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako