• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Tigo Rwanda yaanza kutoa huduma ya 4G kwa wageni wanaotumia huduma ya roaming.

    (GMT+08:00) 2017-05-11 18:52:19

    Kampuni ya kutoa huduma za masiliano ya Tigo nchini Rwanda imeanza kutoa huduma za inaneti ya 4G kwa wageni wanaotumia huduma ya roaming.

    Mkurungezi wa kitengo cha kibiashara nchini humo Yaw Ankoma Agyapong amesema kutokana na kwamba Rwanda inaandaa mikutano mingi ya kimataifa huduma hii imekuja kwa wakati unaofaa.

    Amesema kupitia kwa huduma hii mpya sasa watalii na wafanyabiashara wa kigeni wataweza kutumia mtandao wa kasi.

    Kwa sasa kulingana na kampuni ya Korea Telecom Rwanda Networks (KTRN) matumuzi wa huduma ya 4G imekua kwa zaidi ya asilimia 200% mwaka wa 2016.

    KTRN, imesema huduma hiyo ya 4G inatarjiwa kufikia asilimia 92% mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako