• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Sheria mpya kuwezeha wakenya kupata mikopo kwa kutumia mifugo na mazao

    (GMT+08:00) 2017-05-11 18:58:40

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametia saini kuwa sheria mswada ambao utawezesha wakenya kutumia bidhaa za matumizi ya nyumbani kama runinga kupata mikopo ya benki.

    Pia chini ya sheria hiyo mpya sasa wakenya wataweza kupata mikopo kwa kutumia mazao ya shambani na mifugo.

    Sheria hiyo mpya inatarajiwa kuwasaidia wakenya wasiokuwa na gari au ardhi kupata mikopo.

    Aidha sheria hiyo inawezesha wateja wa benki kutumia bidhaa moja kama gari ama ardhi kupata zaidi ya mkopo mmoja kutoka kwa benki tofauti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako