• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Mumias Sugar yaomba ruzuku ya shilingi milioni 3.4

    (GMT+08:00) 2017-05-11 19:01:10

    Kampuni ya sukari ya Mumias nchini Kenya inaiomba serikali kuipa ruzuku ya shilingi bilioni 3.41 ili kuisaidia kufufua kikamilifu shughuli zake.

    Mwenyekiti wa halmashauri ya kampuni hiyo Kennedy Mulwa amesema pesa hizo zitatumika kulipa madeni kama vile wakulima wanaotoa miwa kwa kiwanda na pia kulipa mishahara ya miezi miwili.

    Kiwanda cha sukari hicho kimefungwa kufanyiwa ukarabati wa kawaida kwa miezi mitatu.

    Bwana Mulwa amekanusa madai kwamba kampuni hiyo imefungwa kutokana na matatizo ya kiedha na kuahidi kwamba watarejelea shughuli za kawaida pindi tu watakuwa na miwa ya kutosha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako