• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Tanzania na Afrika Kusini kuongeza ushirikiano wa uwekezaji

    (GMT+08:00) 2017-05-11 19:01:41

    Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, wa Tanzania Balozi Augustine Mahiga amesema Serikali za Tanzania na Afrika Kusini zimeweka mikakati ya kuongeza maeneo ya ushirikiano, hususan katika biashara na uwekezaji.

    Balozi Mahiga amesema hayo leo alipotoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa mawaziri wa kamisheni ya pamoja ya kitaifa kati ya Tanzania na Afrika Kusini uliofanyika jijini Dar es salaam.

    Naye waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Maite Nkoana -Mashabane ameeleza umuhimu wa kukuza uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya mataifa hayo mawili ili kuwaletea maendeleo wananchi wa mataifa yote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako