• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kujadiliana na wenzi mbalimbali kuhusu mipango wa ushirikiano kwenye kongamano la "Ukanda Mmoja na Njia Moja"

  (GMT+08:00) 2017-05-11 19:04:56

  China itatumia vizuri kongamano la ushirikiano wa kimataifa kuhusu "Ukanda Mmoja na Njia Moja" litakaloanza Jumapili wiki hii, kujadiliana na wenzi mbalimbali kuhusu mipango ya ushirikiano, kujenga jukwaa la wazi kwa pamoja na kunufaika na maendeleo kwa pamoja.

  Akizungumzia kongamano hilo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Geng Shuang amesema hadi sasa, wakuu 29 wa nchi na serikali na wasimamizi watatu wa mashirika ya kimataifa akiwemo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres wamethibitisha kushiriki kwenye mazungumzo ya wakuu ya meza ya duara wakati wa kongamano hilo.

  Bw. Geng pia amesema kongamano hilo litakalohudhuriwa na wajumbe wapatao 1,500 kutoka nchi zaidi ya 130 linajumuisha sehemu tatu za ufunguzi, mkutano wa ngazi ya juu na mazungumzo ya wakuu ya meza ya duara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako