• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raisi wa FIFA aipa tafu Afrika kwa kuipatia nafasi 9 kombe la dunia

    (GMT+08:00) 2017-05-12 08:47:42

    Shirikisho la soka duniani FIFA chini ya raisi wake mpya Gianni Infantino linaonekana kujaribu kuinua sana soka katika ukanda wa Afrika, ambako kuna wafuasi wengi wa Infantino.

    Shirikisho hilo sasa limeamua kuipa Afrika nafasi ya upendeleo kwa kuiongezea nafasi 5 zaidi za ushiriki katika fainali za kombe la dunia la mwaka 2026. Katika fainali hizo timu zitaongezeka kutoka 36 hadi 48 na Afrika itawakilishwa na timu 9 ambapo nyingine ya 10 itapambana katika hatua ya mtoano.

    Shirikisho hilo pia limeongeza idadi ya timu katika bara la Ulaya ambapo mwanzoni zilikuwa ni timu 13 na sasa zitakuwa 16, huku Marekani Kaskazini na kusini zikiwa timu 6 badala ya 3.

    Oceania nao wamepewa nafasi moja ya uwakilishi wa moja kwa moja ambapo hapo mwanzo iliwapasa wacheze mchezo wa mtoano na timu za Amerika Kusini ili kufuzu.

    Hii itawafanya New Zealand kuwa na nafasi kubwa ya kushiriki kombe la dunia kila mara kutokana na kutokuwa na upinzani mkubwa haswa baada ya Australia kuanza kushiriki michuano ya bara la Asia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako