• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kagera Sugar yaitaka Simba iseme ukweli kuhusu mshambuliaji Mbaraka Yussuf Abeid

    (GMT+08:00) 2017-05-12 08:48:26

    Uongozi wa Kagera Sugar kupitia Meneja wake Mohammed Hussein Umeitaka klabu ya Simba SC iseme ukweli kwa umma kuwa mshambuliaji Mbaraka Yussuf Abeid walimtoa kwa mkopo na wala siyo kwa mkataba wowote kama wao wenyewe wanavyodai. Hussein amebainisha hayo baada ya Rais wa Simba SC, Evans Aveva kusema wataenda kufungua kesi mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) dhidi ya klabu hiyo kwa madai ya kuwadhulumu mchezaji wao Mbaraka Yussuf waliyempeleka kwa mkopo lakini timu hiyo ikajimilikisha moja kwa moja kinyume cha sheria na makubaliano waliyowekeana.

    Aidha Hussein ameedelea kubainisha baadhi ya mambo kwa kusema baada ya kumalizika msimu uliopita, Simba walimuhitaji Mbaraka Yussuf Abeid arejee msimbazi lakini mchezaji mwenyewe akagoma na kusema hakuwahi kusaini mkataba wowote na Wekundu hao wa msimbazi.

    Pamoja na hayo Hussein amesema waliweza kufuatilia suala hilo katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kujiridhisha kwamba kweli mchezaji huyo hakuwa na mkataba wowote katika kipindi hicho na kuamua kumpa wa kwao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako