• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Kagame aonesha kutoridhishwa na kasi ndogo ya kuanzishwa kwa eneo moja la mtandao wa simu

    (GMT+08:00) 2017-05-12 09:32:06

    Rais Paul Kagame wa Rwanda ameonesha kutoridhishwa na kasi ndogo ya kuanzishwa kwa eneo moja la mtandao wa simu barani Afrika kwa lengo la kupunguza gharama za simu za kimataifa.

    Akiongea kwenye mkutano wa Transform Afrika unaofanyika mjini Kigali, Rais Kagame amesema kucheleweshwa huko hakujatokana na ukosefu wa teknolojia, bali ni uelewa.

    Eneo moja la mtandao wa simu linahusisha nchi ambazo zimekubaliana kuondoa kodi za ziada kwenye simu za kimataifa baina yao. Kwa sasa lina nchi nne za jumuiya ya Afrika Mashariki, yaani Kenya, Uganda, Rwanda na Sudan Kusini.

    Habari pia zinasema Rwanda imesaini makubaliano na shirika la mawasiliano ya satellite Inmarsat, ili kuboresha huduma za kidigitali nchini Rwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako