• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 51 wafa kwa kipindupindu Yemen ndani ya wiki mbili

    (GMT+08:00) 2017-05-12 09:42:49

    Taarifa iliyotolewa na Shirika la afya duniani WHO inasema, mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen umesababisha vifo vya watu 51 ndani ya wiki mbili. Kesi zaidi ya 2,700 za maambukizi zimeripotiwa tangu Aprili 27 katika mikoa 10 nchini humo, ikiwemo mji mkuu Sanaa. Mwakilishi wa WHO nchini Yemen Dk. Nevio Zagaria ametoa mwito wa hatua madhubuti kuchukuliwa ili kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo nchini humo, ambako mfumo na miundombinu ya afya imeharibiwa vibaya katika machafuko yaliyodumu kwa miaka miwili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako