• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe maalumu wa UM asema duru mpya ya mazungumzo ya suala la Syria inatakiwa kuwa na matokeo halisi

    (GMT+08:00) 2017-05-12 10:08:05
    Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Syria Bw. Staffan de Mistura, jana alisema mjini Geneva kuwa duru mpya ya mazungumzo ya amani ya Geneva inatarajiwa kupata matokeo halisi kama iwezekanavyo, kwenye msingi wa makubaliano yaliyofikiwa kwenye mazungumzo ya Astana, na kwamba serikali ya Syria na waasi watasitisha mapambano kwa miezi 6 katika maeneo manne nchini Syria, lakini mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi yataendelea.

    Bw. Staffan de Mistura amesema mazungumzo ya duru hii yatakayomalizika tarehe 19 mwezi huu yanatarajiwa kuwa na matokeo ya kuridhisha. Mazungumzo ya duru ya tano yaliyofanyika mwezi wa Machi mjini Geneva hayakufikia makubaliano yoyote ya amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako