• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasaini makubaliano ya ushirikiano wa kiutamaduni na nchi zaidi ya 60 za "Ukanda mmoja na njia moja"

    (GMT+08:00) 2017-05-12 10:11:04

    Naibu waziri wa utamaduni wa China Bw Ding Wei amesema kwamba hadi kufikia mwaka jana, China ilikuwa imesaini makubaliano ya ushirikiano wa kiutamaduni na nchi zaidi ya 60 za "Ukanda mmoja na njia moja".

    Amesema China imeanzisha taratibu za mazungumzo wa kikanda na nchi za "Ukanda mmoja na njia moja", ili kufanikisha ushirikiano huo. Ameongeza kwamba ushirikiano wa "Ukanda mmoja, njia moja" pia unahitaji ushiriki wa mashirika ya kijamii.

    Kwa upande wa mawasiliano ya watu, China inafanya juhudi kuanzisha miradi mbalimabli ya kiutamaduni, na kupanga kuwashirikisha watu elfu 30 kwenye shughuli za mawasiliano ya kiutamaduni kabla ya mwaka 2020.

    Hadi sasa, vituo 11 vya utamaduni wa China vimezinduliwa katika nchi za "Ukanda mmoja, njia moja", na vituo vingine 13 vitajengwa ndani ya miaka mitatu hadi minne ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako