• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China itaendelea kushirikiana na nchi nyingine katika mapambano dhidi ya ugaidi

    (GMT+08:00) 2017-05-12 16:53:42

    Naibu balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa Wu Haitao amesema China itaendelea kushirikiana na nchi nyingine katika mapambano dhidi ya ugaidi na kulinda amani na utulivu duniani.

    Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika jana mjini New York, Bw. Wu amesema makundi ya IS na Al- Qaeda yanatishia amani na usalama wa kimataifa, na uwezo wa nchi mbalimbali wa kupambana na ugaidi na ushirikiano wa kimataifa katika sekta hiyo vinapaswa kuimarishwa. Pia amesema China inaunga mkono kamati ya kupambana na ugaidi ya Umoja wa Mataifa kuendelea kufuatilia suala la makundi ya kigaidi kukusanya fedha na kufanya shughuli za kigaidi kwenye mtandao wa internet.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako