• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China na Burundi zaahidi kuunganisha mikakati ya maendeleo na kuimarisha ushirikiano

  (GMT+08:00) 2017-05-12 17:00:17

  Viongozi wa Burundi na China wameahidi kuunganisha mikakati ya maendeleo ya nchi hizo mbili na kuimarisha uhusiano wao, zikilenga maeneo ya kilimo na miundombinu.

  Ahadi hiyo ilitolewa wakati wa mkutano kati ya rais Pierre Nkurunziza wa Burundi na makamu wa rais wa China Li Yuanchao ambaye yuko ziarani nchini Burundi. Rais Nkurunziza amesisitiza tena kuwa Burundi inaunga mkono sera ya China moja, na msimamo wa China kuhusu suala la Bahari ya Kusini ya China na Peninsula ya Korea.

  Kwa upande wake, makamu wa rais Li amesema ziara yake inalenga kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na rais Xi Jinping wa China na rais Nkurunziza wakati wa mkutano wao uliofanyika kando ya Mashindano ya Olimpiki ya Majira ya Joto kwa vijana mjini Nanjing, mashariki mwa China mwaka 2014.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako