• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi wa bomba la gesi wa Afrika Magharibi kuongezewa nguvu

    (GMT+08:00) 2017-05-12 17:00:44

    Mkutano wa kikanda unatarajiwa kufanyika leo mjini Cotonou, Benin, kwa lengo la kuondoa vikwazo vinavyozuia utendaji mzuri wa mradi wa bomba la gesi wa Afrika Magharibi, WAGP.

    Taarifa rasmi iliyotolewa mjini Cotonou imesema, kamati ya mawaziri wa WAGP itakutana na kamishna wa nishati na madini wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS kujadili suala hilo. Taarifa hiyo imesema, mkutano huo umeitishwa na waziri wa nishati na madini wa Benin, na unalenga kutafuta njia na mbinu za kuondoa vizuizi vinavyozuia uendeshaji mzuri wa mradi huo.

    Mradi wa bomba la gesi wa Afrika Magharibi WAGP unajumuisha nchi za Benin, Togo, Ghana na Nigeria, na unalenga kuwa mtoaji mkuu wa rasilimali ya gesi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako