• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Upepo mkali waleta ukame wa maji mashariki mwa DRC

  (GMT+08:00) 2017-05-12 19:01:57

  Changamoto kubwa yakupata maji kwa matumizi ya nyumbani;yawakumba wakaaji wa mashariki ya jamhuri ya kideokrasia ya Congo;kwa upeke tukizungumuzia mkoa wa kivu ya kaskazini sehemu yake ya kaskazini;na pia mkoa wa Ituri;maeneo ambayo upepo mkali umevuma la kupita kiasi na kupelekea ukame.hata maboma yamekosa maji na kupelekea wanawake wengi kama vile wanaume;hata vijana kuangaika kutafuta maji kinyume na saa zinazofaa.hali inayoleta hofu haswa kulingana na ukosefu wa usalama majira ya usiku.

  Ni tangu mwezi wa machi mwishoni mwake;kuingia Aprili hadi kufikia May hii ikiwa ni apatao mwezi mmoja na nusu;upepo mkali unashuhudiwa ;na kusababisha vumbi nyingi inayowasumuwa wakaaji na kuleta hata wasiwasi mkubwa miongoni mwa raia;kwa kuwa kuna paa nyingi za nyumba za wakaaji zilizorushwa;mashule kama vile makanisa hayakuachwa nyuma.

  Ajabu ni kwamba;hata maji kwenye mabomba ya umaa;huwa umaliza siku mbili bila yakutokea,na kuhathiri maisha ya kawaida ya wakaaji kwa mahitaji ya nyumbani.

  Niliwafikia mama moja aliye mzaifu kwa jia la ASHA;pamoja na msichana mwengine kwa jina la CHARMANTE MANGAYA;lakini huyo wa kwanza,licha ya magonjwa;amehamka saa tano za usiku kuenda kutafuta maji;au kwenye visima;au kwenye mabomba ya umaa yaliyojengwa katika ushirikiano kati ya serkali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na shirika moja la kimataifa lisilokuwa la kiserkali toka Ufaransa kwa jina la SOLIDARITE;na vilevile msichana niliye kutana naye;wote wawili;mmoja baada ya mwengine;walikuwa na haya ya kuzungumza:

  "Mimi ninaumwa;lakini najitaidi kuhamka saa tano za usiku kutafuta maji lakini unapo pafika huwa hutapata,unasubiri saa nane au saa ktisa za usiku ndiyo utapata maji;na kukosekana kwa maji ni kutokana na upepo mkali unao vuma ambao ndiyo unaofikiriwa kuwa chanzo cha magumu yote kwasababu maji yamekauka…" "

  Hata hivyo Nilifunga safari hadi kwenye mabomba yanayojengwa sehemu za umaa;nikamfikia muhuduma aliyewekwa mahali hapo kwa ajili ya ulinzi pamoja na kuwatolea watu maji kati ya zaidi ya mabomba 100 katika mradi uliyo julikana kama Fontaines 100.Nilimuuliza baba huyu ambaye hakutaka jina lake litajwe;je,anaweza kunifasiria machache kuhusu mwenendo wa huduma za maji kwa sasa?Huyu aliniambia:

  "Hakika;watu wanateseka;na hiyo ni kutokana na upepo katika mji wetu wa Beni.Tunamaliza hata siku mbili bila yakupata maji;vumbi vivyohivyo;hata wamama wanalala nje kutafuta maji.Wengi wachelewa kuenda kazini kwa kutafuta maji.Hakika watu wanateseka…"

  Ilitubidi kuwa tafuta wakuu husika wanaogawa maji kwa wakaaji;minajili ya kupata habari sahii kuhusiana na hali hiyo;bila yakuta sauti zao zinaswe;walidokeza kwamba hali hiyo ni yakawaida kwa kuwa maji yamepunguka sehemu zinazozalisha na kusukumia mirija;ikionekana kwamba;maji yameshuka toka mahli pake pakila siku;nayo mirija yamebaki juu yakiachana kwa kuwa tupo katika msimu wa juwa;na ni upepo mkali unayosababisha ukame.

  Ni hayo ndugu mwenye kiti.Leo tulimulika hali ya ukame inayokausha maji kwenye mabomba;na kupelekea wakaaji wa mashariki mwa Congo-kinshasa;kusumbuka na maji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako