• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wazitaka pande husika zifanye juhudi za pamoja ili kukomesha mgogoro nchini Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2017-05-13 16:37:40

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres anaitaka pande husika zifanye juhudi za pamoja, ili kukomesha mgogoro nchini Sudan Kusini.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Guterres amesema hayo baada ya kukutana na wawakilishi wa Mamlaka ya Maendeleo ya kitaifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki IGAD na Umoja wa Afrika kuhusu suala la Sudan Kusini.

    Katika mazungumzo hayo, Bw. Guterres ana wasiwasi kuhusu hali ya usalama na hali ya kibinadamu nchini Sudan Kusini, na kusisitiza kuwa kanda hiyo na jumuiya ya kimataifa zinapaswa kufanya juhudi za pamoja kuhimiza usimamishaji wa vita ili kuhakikisha njia iko wazi kwa utoaji wa misaada ya kibinadamu, na tume maalumu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini kuweza kusafiri huru, na kuhimiza mchakato wa kisiasa yenye uvumilivu na uaminifu, na kuondoa mgogoro nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako