• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bw. Li Keqiang akutana na waziri mkuu wa Ethiopia

  (GMT+08:00) 2017-05-13 16:59:41

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana alasiri amekutana na waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Hailemariam Dessalegn ambaye atahudhuria mkutano wa kilele wa baraza la ushirikiano wa kimataifa kuhusu "Ukanda mmoja na Njia moja" hapa Beijing.

  Bw. Li amesema China inapenda kushirikiana na Ethiopia, kuimarisha uaminifu wa siasa, kupanua ushirikiano wa ufanisi, na kuhimiza maendeleo ya mipango kumi ya ushirikiano kati ya China na Afrika na ushirikiano wa viwanda kati yao.

  Bw. Hailemariam amesema, Afrika na China zina lengo la pamoja la maendeleo. Ethiopia inafanya juhudi kujenga kituo cha usafiri wa anga cha kikanda, na inapenda kufikiria kununua ndege kubwa zilizotengenezwa na China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako