• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR yafungua kambi ya 12 ya wakimbizi nchini Iraq kwa ajili ya makazi ya familia waliokimbia Mosul

    (GMT+08:00) 2017-05-13 17:23:41

    Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) wiki hii limefungua kambi mpya kwa ajili ya makazi kaskazini mwa Iraq kutokana na kuongezeka kwa idadi ya familia kutokana na kukimbia mapigano magharibi mwa Mosul.

    Msemaji wa shirika hilo Andrej Mahecic aliwaambia waandishi wa habari kwamba, kambi 12 za aina hiyo zimetengwa kutokana hali ya dharula inayoendelea mjini Mosul, ilikuwa kilomita 60 magharibi mwa Mosul katika njia kuu ya Erbil.

    Alisema kuwa katika eneo hilo jipya limehifadhi karibu watoto 500, wanawake na wanaume na kufanya jumla ya familia 96 zilizohifadhiwa. Eneo hilo lina uwezo wa kuhifadhi watu zaidi ya 9,000 kwa kikamilifu.

    UNHCR imesema kuwa, hatari kwa watu waliokimbia Mosul ni kubwa sana, familia huwasili kutoka Mosul ikikimbia mapigano makali na kueleza kuwa hakukuwa na huduma za msingi katika mji.

    Kwa mujibu wa viongozi wa Iraq, zaidi ya watu 630,000 wameyakimbia makazi yao kutokana na Mosoul na maeneo ya jirani tangu Oktoba 2016 wakati operesheni ya kijeshi ilipoanza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako