• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tapio Laukkanen ashinda taji mbio za magari Eldoret

    (GMT+08:00) 2017-05-15 08:33:04
    Dereva Tapio Laukkanen kutoka Finland amedhihirisha kuwa hakubahatisha kushinda mataji ya Mbio za Magari za duru ya Eldoret mwaka 2015 na 2016 baada ya kuendelea kushinda taji hilo mwaka huu katika mashindano ya magari yaliyofanyika jumamosi mjini Eldoret Kenya.

    Miongoni mwa madereva walioonyeshwa kivumbi na bingwa huyu wa Kenya mwaka 2016 ni mshindi wa Kenya na Afrika mwaka 2015 Jaspreet Chatthe pamoja na bingwa wa zamani wa Kenya, Baldev Chager.

    Baada ya ushindi wake huo, Tapio amemshukuru muelekezi wake Gavin Laurence kwa kumpatia maelekezo mazuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako