• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanariadha wa Kenya ashindwa mbio za China

    (GMT+08:00) 2017-05-15 08:33:50
    Bingwa mara mbili wa michezo ya Olimpiki mbio za mita 800 David Rudisha ameanza vibaya msimu mpya wa riadha hapa China Jumamosi lakini Wakenya wenzake Faith Kipyegon na Hellen Obiri wakaibuka washindi kwenye mbio zao.

    Akishiriki katika mkondo wa pili wa mfululizo wa mashindano ya Golden League, Rudisha, ambaye anashikilia rekodi ya dunia, alimaliza wa 4 kwa muda wa 1:45:36

    Wakenya wenzake walichukua nafasi tatu za mwanzo wakiongozwa na Kipyegon Bett aliyetumia 1:44:70 akifuatiwa na Robert Biwott na Ferguson Rotich.

    Rudisha amesema matokeo hayo mabovu ni kwa sababu hajakimbia kwa muda mrefu tangu mwaka jana aliposhinda dhahabu yake ya pili katika michezo ya Olimpiki mjini Rio de Janeiro.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako