• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yasema ripoti ya CIA ni ishara nzuri ya kuondoa vikwazo vyote

    (GMT+08:00) 2017-05-15 09:07:01

    Serikali ya Sudan imesema inaamini kuwa vikwazo vyote vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Sudan vitaondolewa, baada ya ripoti ya shirika la ujasusi la Marekani CIA kusema serikali ya Sudan imetimiza vigezo vyote.

    Waziri wa habari wa Sudan Bw Ahmed Bilal Osman ametaja ripoti hiyo ya CIA kuwa ni "ishara chanya", na kueleza imani yake kuwa bunge la Marekani na Rais wa Marekani wataondoa vikwazo vyote dhidi ya Sudan. Pia amesema Sudan inatoa ushirikiano kwa pande zote, kwa hiyo ni hali ya kawaida kwa vikwazo kuondolewa.

    Hapo awali serikali ya Marekani ilitoa masharti ya kuondoa vikwazo vyote dhidi ya Sudan, yanayoitaka nchi hiyo kutoa ripoti kabla ya Julai 12 ikiahidi kupambana na ugaidi na kukomesha uhasama kwenye maeneo yenye mapambano.

    Mwaka 1993 Marekani iliiweka Sudan kwenye orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi, na mwaka 1997 iliiwekea nchi hiyo vikwazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako