• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama cha CDU cha Ujerumani kinaonekana kushinda uchaguzi katika jimbo muhimu

    (GMT+08:00) 2017-05-15 09:36:03
    Makadirio baada ya upigaji kura jimbo Rhine-Westphalia kaskazini mwa Ujerumani yanaonesha kuwa chama cha chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel CDU kimeshinda kwenye uchaguzi.

    Kutokana na makadirio yaliyotolewa na vyombo vya habari, chama cha CDU kinatarajiwa kupata asilimia 34 ya kura, chama cha SPD kinatarajiwa kupata asilimia 30.6 ya kura. Uchaguzi wa jana utakuwa uchaguzi wa mwisho kwenye majimbo yenye ushindani mkali kati ya Bibi Merkel na mwenyekiti wa SPD Bw. Martin Schulz kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Septemba 24.

    Matokeo hayo yanaweza kuongeza imani ya CDU kwenye uchaguzi mkuu baada ya kuwa na ushindi kwenye majimbo, licha ya kuwa uungaji mkono kwa chama cha SPD umeongezeka, kufuatia kushuka kwa imani na Bibi Merkel kutokana na sera yake ya suala la wakimbizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako