• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bw. Wang Yi akutana na mwenzake wa Kenya Bibi Amina Mohamed

  (GMT+08:00) 2017-05-15 10:09:28

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana hapa Beijing alikutana na mwenzake wa Kenya Bibi Amina Mohamed ambaye yuko Beijing kuhudhuria mkutano wa kilele wa Baraza la "Ukanda mmoja na Njia moja".

  Bw. Wang Yi amesema, rais Xi Jinping wa China akihutubia ufunguzi wa mkutano huo, amesema "Ukanda mmoja na Njia moja" utajengwa kuwa njia yenye amani, ustawi, uwazi, uvumbuzi na utamaduni, na itatoa mwelekeo katika kuimarisha ushirikiano wa kimataifa ikiwemo ushirikiano kati ya China na Afrika.

  Bw. Wang Yi amesema Kenya ni nchi muhimu barani Afrika na ni mfano wa kuigwa wa ushirikiano wa kiviwanda kati ya China na Afrika. Pia ameeleza imani yake kuwa Kenya inaweza kupata maendeleo ya kasi kwenye mchakato wa ujenzi wa "Ukanda mmoja na Njia moja."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako