• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msingi wa uhusiano wa nchi ni maelewano ya watu-----mahojiano na waigizaji wa sauti za tamthilia za kichina kutoka Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-05-15 16:31:31

    Mkutano wenye kaulimbiu ya "kuzidisha maelewano ya watu" umefanyika pembezoni mwa kongamano la ushirikiano wa kimataifa la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" linaloendelea hapa Beijing, China, ambapo waigizaji wa sauti wa kampuni ya StarTimes kutoka Tanzania walitoa mfano jinsi walivyotia sauti kwenye tamthilia ya kichina "mfalme kima", na maonyesho yao yalivutia makofi mengi kutoka washiriki wa mkutano huo.

    Hilda Malecela ni mmoja wa waigizaji hao, na sasa anafanya kazi ya kutilia sauti kwenye tamthilia za kichina kwa lugha ya Kiswahili. Mwaka 2011, tamthilia ya kichina "Doudou na Mama Wakwe Zake" ilionyeshwa nchini Tanzania, kuanzia hapo Hilda Malecela akawa shabiki mkubwa wa tamthilia ya kichina.

    Alipoeleza pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", rais Xi Jinping wa China alitaja mara nyingi kuwa "msingi wa uhusiano wa nchi ni maelewano ya watu". Mawasiliano ya kitamaduni yamekuwa daraja na kiunganishi katika kuongeza maelewano ya watu. Ili kuwafanya watu wa nje kuielewa zaidi China na kuongeza maelewano hayo, China imefanya kazi nyingi katika miaka mingi iliyopita, ikiwa ni pamoja na kutafsiri na kutia sauti kwa lugha mbalimbali tamthilia za kichina na kuzionyesha katika nchi za nje. Hilda Malecela anaona kuwa hatua hiyo imehimiza mawasiliano ya kitamaduni kati ya China na nchi nyingine.

    Kutokana na kwamba tamthilia za Kichina zina soko kubwa katika nchi zinazotumia lugha Kiswahili za Afrika Mashariki na Kati, waigizaji wa sauti wa lugha ya Kiswahili wanahitajika sana, kwa hivyo wengi wamekuja China kutoka Tanzania kufanya kazi husika. Mwigizaji mwingine wa kampuni ya StarTimes Abdul Maisala Lihinda sasa yupo Beijing, na hii ni mara yake ya pili kuja China kufanya kazi za kutia sauti tamthilia za kichina.

    Mwaka jana, Abdul Maisala Lihinda alishiriki kwenye shindano la kutia sauti lililoandaliwa na kampuni ya StarTimes nchini Tanzania, na kutokana na kupata alama nzuri, alipewa nafasi ya kuja kufanya kazi hapa China hivi sasa, tamthilia za kichina alizoshiriki kutia sauti zinaonyeshwa Tanzania, Burundi, Kenya na nyingine zinazotumia lugha ya Kiswahili. Akizungumzia maisha yake ya miaka kadhaa iliyopita, Bw Maisala amesema amejifunza mengi na atayatumia baada ya kurudi nyumbani ili kunufaisha taifa lake.

    Maelewano ya watu ni msingi wa jamii na watu katika pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na yanaweza kuongeza urafiki kati ya watu wa nchi zilizojumuishwa na pendekezo hilo, na pia yanasaidia kuhimiza ushirikiano kati ya nchi hizo katika sera, vifaa, biashara na fedha. Inaaminika kuwa kama maelewano ya watu yataimarika, makubaliano yatakapatikana duniani kuhusu kuthamini amani, ushirikiano na mafanikio ya pamoja kutokana na ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako