• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kusini kupeleka wajumbe maalum nchini China, Marekani, Russia, Japan na Umoja wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2017-05-15 18:40:32

    Rais Moon Jei-in wa Korea Kusini ameteua wawakilishi maalum watakaopelekwa nchini China, Marekani, Russia, Japan, na Umoja wa Ulaya.

    Ofisi ya rais ikulu imesema katika taarifa yake iliyotolewa leo kuwa, rais Moon ameteua watu wanaoelewa vizuri zaidi mtazamo wake wa kidiplomasia na sera za kigeni.

    Mara baada ya kushinda katika uchaguzi wa rais, Moon aliwasiliana kwa njia ya simu na viongozi mbalimbali wa nchi zenye nguvu duniani na kuahidi kupeleka wajumbe maalum kwa ajili ya majadiliano kuhusu hali ya sasa katika Peninsula ya Korea.

    Rais Moon amemteua waziri mkuu Lee Hae-chan, kuwa mjumbe wake maalum nchini China kuhusu mfumo wa THAAD wa Marekani na Korea Kaskazini, kwa kuwa masuala hayo mawili yanaingiliana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako