• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaongeza ulinzi wa mtandao wa internet wakati wa tishio la shambulizi la mtandao

  (GMT+08:00) 2017-05-15 18:40:56

  Mamlaka ya Usimamizi wa Mtandao wa Internet ya China (CAC) imewaonya watu wanaotumia kompyuta kuweka na kuimarisha programu ya usalama wa kompyuta ili kuepuka mashambulizi kwenye mtandao.

  Polisi na mamlaka mbalimbali za serikali zimechukua hatua za kujihami dhidi ya shambulizi la mtandao wa internet linaloikabili dunia, na kampuni za usalama wa internet ikiwemo Qihoo 360 pia zimeongeza huduma za usalama. Akaunti 18,000 nchini China zimethibitika kuathiriwa na shambulizi hilo liitwalo "WannaCry", ambalo lilianza kusambaa duniani ijumaa iliyopita.

  Mamlaka hiyo imesema, kwa mara nyingine tena shambulizi hilo limeonyesha changamoto zisizotarajiwa za kiusalama kwenye mtandao wa internet, na kutoa wito kwa sekta zote husika kukabiliana na masuala ya usalama wa mtandao wa internet.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako