• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Bei ya petroli, mafuta –taa yaongezeka, dizeli yashuka

    (GMT+08:00) 2017-05-15 19:23:23

    Tume ya Kudhibiti Kawi nchini (ERC) imetangaza bei mpya za mafuta, ambapo petroli itauzwa kwa sh99.59 jiini Nairobi.

    Hili ongezeko la sh1.59, ambapo ilikuwa ikiuzwa kwa sh98.00.

    Kwenye tangazo tangazo hilo jana, bei mpya ya dizeli itakuwa sh88.05 huku ya mafuta ikiwa sh65.28.

    Aidha, bei hizo ni upungufu wa sh0.57 na ongezeko la sh0.90 mtawalia.

    Mjini Mombasa, petrol itauzwa kwa sh96.32, dizeli sh84.79 huku mafuta taa yakiuzwa kwa sh65.28.

    Kulingana na mkurugenzi mkuu wa tume hiyo Bi Mueni Mutunga, bei hizo mpya zinatokanana mabadiliko ya mafuta katika soko la Kimataifa.

    Aidha, mabadiliko hayo yatatekelezwa kuanzia leo hadi Juni tarehe 14.

    Tume hiyo pia iliwaonya wamiliki wa viwanda vya mafuta kuzingatia bei hizo mpya, la sivyo wachukuliwe hatua.

    Lakini licha ya mabadiliko hayo yanaonekana kutopunguza hali ngumu ya maisha nchini

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako