• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania Serikali kugawa bure pembejeo za korosho

    (GMT+08:00) 2017-05-15 19:24:13

    SERIKALI imetangaza rasmi kugawa pembejeo za korosho bure kuanzia Msimu wa Kilimo ujao.

    Wakulima watapata bure pembejeo aina ya salfa zilizokuwa zikiuzwa kwa bei ya ruzuku.

    Kauli hiyo ya Serikali ilitolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa anafungua mkutano wa kila mwaka wa wadau wa korosho uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma.

    Aidha amesema nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha vikwazo vyote vilivyokuwa vinawakabili wakulima wa zao hilo vinaondolewa ili kuwawezesha kupata tija zaidi kutokana na zao lao.

    Lengo la Serikali ni kuona mashamba yaliyotelekezwa na yenye mikorosho iliyozeeka yanafufuliwa ili kuongeza uzalishaji na kukuza uchumi wa wakulima na nchi kujipatia kipato cha kutosha.

    Mikorosho asilimia 25 iliyopo sasa ni ile iliyozeeka ambayo haizalishi kiasi cha kuridhisha.

    Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Nchini (CBT), Anna Abdallah, amesema bodi hiyo imenunua tani 18,000 za pembejeo aina ya Salfa.

    Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ushirika, Dk Charles Tizeba alitoa taarifa za mapato yatokanayo na mazao ya biashara, na amesema korosho imeongoza kwa kuliingizia taifa fedha za kigeni kutokana na mauzo ya nje ya zao hilo katika msimu uliopita.

    Tizeba amesema jumla ya dola za kimarekani ni milioni 300.46 (sh bilioni 630.9) ambazo zilipatikana kutokana na mauzo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako