Ushirikiano kati ya China na Kenya waingia kwenye njia ya kasi
Reli ya SGR kutoka Mombasa kwenda Nairobi, ambayo ni reli ya kwanza iliyojengwa tangu Kenya ipate uhuru, inatarajiwa kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi huu. Reli hiyo inayoitwa na wakenya "ujenzi wa milenia" imejengwa kwa kufuata vigezo vya kichina, na inabeba ndoto ya watu wa vizazi vilivyopita vya Kenya, na kusaidia kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii ya Afrika Mashariki kuingia kwenye njia ya kasi.
|