• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Fainali za mataifa ya Afrika: U-17, Serengeti Boys yailazimisha sare mabingwa watetezi

    (GMT+08:00) 2017-05-16 08:34:51
    Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imegawana pointi na mabingwa watetezi, Mali katika mchezo wa kwanza wa kundi B Fainali za Mataifa ya Afrika jioni ya jana uwanja wa l'Amitie Sino mjini Libreville, Gabon.

    Mali walimiliki mpira kwa muda mrefu na kupanga vyema mashambulizi yao, lakini safu ya ulinzi ya Tanzania ilicheza vizuri na kuokoa hatari nyingi ukiacha chache ambazo mabingwa hao watetezi walipoteza wenyewe.

    Mchezo wa pili wa Kundi B ulifuatia jioni ya jana kati ya Niger na Angola baada ya mechi za Kundi A kuchezwa jana Uwanja wa Port Gentil jana wenyeji Gabon wakifungwa mabao 5-1 na Guinea huku Ghana wakianza vizuri kwa ushindi wa 4-0 dhidi ya Cameroon.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako