• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi Kuu Kenya-KPL: Stewart Hall hofu yazidi kumpanda baada ya matokeo mabaya, agomea waandishi wa habari

    (GMT+08:00) 2017-05-16 08:35:17
    Hofu imeanza kumpanda kocha wa AFC Leopards, Stewart Hall kama alivyoonekana wikiendi baada ya timu yake kushindwa kupata ushindi kwenye mechi ya tatu mfululizo.

    Mara tu kipenga cha kuumaliza mchezo waliolazimisha sare ya 1-1 na Zoo Kericho kupulizwa uwanjani Machakos, Hall aliondoka huku akikataa kuzungumza na wanahabari, ikiwa ni tofauti na ilivyo desturi yake ambapo huingia uwanjani kupongeza wachezaji wake kisha wakaondoka.

    Hiyo ilikuwa mechi ya tatu mfululizo kwa AFC Leopards kutopata ushindi, baada ya kupokea kichapo kwa watani wao wa jadi Gor Mahia, na kisha kufungwa na Sony Sugar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako