Shirika la umeme la Msumbiji limesema watu wapatao milioni 25 nchini humo watanufaika na mpango wa upanuzi wa gridi ya taifa unaolenga kuunganisha maeneo mengi zaidi mijini na vijijini. Ofisa wa shirika hilo Pascoal Bassela amesema shirika hilo litawekeza dola milioni 100 za kimarekani kila mwaka katika kupanua mtandao wa umeme, ambao unatarajiwa kufika maeneo ya nchi nzima ifikapo mwaka 2030, na kutoa huduma za umeme kwa kila familia nchini humo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |