• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Kenya kuimarisha uhifadhi wa aina mbalimbali za mimea

    (GMT+08:00) 2017-05-16 09:31:53

    China na Kenya zitaimarisha ushirikiano kwenye utafiti wa kisayansi na kuendeleza uwezo wa kuimarisha uhifadhi wa mimea pori nchini Kenya.

    Mkuu wa Kituo cha utafiti cha pamoja cha China na Afrika Bw Wang Qingfeng, amesema China iko tayari kuisidia Kenya kuwa na uwezo wa usimamizi endelevu wa mimea yake. Amesema tangu miaka mitano waliposaini makubaliano na Makumbusho ya taifa ya Kenya, wameimarisha utafiti wa pamoja ili kulinda mimea mbalimbali.

    Bw Wang amesema kwa sasa jamii zinajielekeza kwenye mimea ya asili kwa ajili ya maliasili, dawa, nishati na chakula, hali inayofanya kuwe na haja ya kuwepo kwa juhudi za kulima mimea hiyo.

    Kenya ni moja ya nchi za Afrika zinazonufaika na uungaji mkono wa kiufundi na kifedha kutoka kwa China, kwenye kuimarisha uhifadhi wa viumbe na wanyamapori.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako