• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujerumani na Ufaransa kuweka kwa pamoja mpango wa mageuzi ya Umoja wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2017-05-16 09:38:32

    Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel jana huko Berlin alikutana na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na kufanya naye mazungumzo. Baada ya mazungumzo yao, wakuu hao wawili wameamua kuhimiza utungaji wa mpango wa mageuzi ya Umoja wa Ulaya, ili kusisitiza mwekeleo wa mshikamano na maendeleo ya Umoja huo baada ya Uingereza kujitoa kutoka umoja huo. Ujerumani na Ufaransa pia zitafanya mkutano wa mawaziri kuhusu suala hilo mwezi Julai.

    Chansela Merkel amesema miradi ya ushirikiano kati ya Ujerumani na Ufaransa kama vile uratibu wa sera za ushuru, itasaidia kuongeza nguvu ya mshikamano ndani ya Umoja wa Ulaya. Pande hizo mbili pia zimekubali kurekebisha mikataba ya Umoja wa Ulaya wakati wa lazima.

    Habari pia zinasema, rais Macron amemteua Bw. Edouard Philippe kuwa waziri mkuu wa Ufaransa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako