• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya asema ruwaza ya China inakidhi mahitaji ya maendeleo Afrika

    (GMT+08:00) 2017-05-16 09:55:11

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema ruwaza ya China ya kuunganisha dunia kwa kuimarisha biashara inakidhi mahitaji ya Afrika ya kuwa na ustawi wa pamoja.

    Akiongea kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ukanda wa Mmoja, Njia moja uliofungwa jana hapa Beijing, Rais Kenyatta amesema Afrika ina nafasi ya kurejesha tena fursa ilizokosa kutokana na utandawazi, kwa kushiriki kikamilifu kwenye mpango wa China wa kuunganisha dunia.

    Rais Kenyatta amesema njia ya Hariri iliyoanzishwa na China inafaa katika ajenda za Umoja wa Afrika katika kujenga miundombinu zaidi inayounganisha bara zima. Pia amesema rais Xi Jinping ni rafiki wa kweli wa Kenya na amekuwa akiisaidia nchi hiyo kwenye juhudi za mageuzi. Ametaja ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kuwa umeonesha uwezekano mkubwa wa ushirikiano wa kunufaishana kati ya Kenya na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako