• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa mataifa una imani kuwa serikali ya Syria inaweza kutatua mgogoro kwa njia ya kisiasa

  (GMT+08:00) 2017-05-16 10:02:55
  Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Bw. Staffan de Mistura amesema anaamini kuwa serikali ya Syria ina nia ya kusitisha mapigano na kutatua migogoro kwa njia ya kisiasa. Bw Mistura amesema hayo wakati ujumbe wa serikali ya Syria wenye watu zaidi ya 18 umefika Geneva kushiriki kwenye duru mpya ya mazungumzo ya amani.

  Hata hivyo amekanusha taarifa inayodai kuwa ushiriki wa serikali ya Syria kwenye mazungumzo hayo unalenga kufunika operesheni kubwa zaidi ya kijeshi nchini humo, na kusema mazungumzo ya amani ya Geneva si mazungumzo matupu bali ni mchakato muhimu wa kisiasa wa kuleta amani nchini Syria. Na ajenda ya mazungumzo itakuwa ni kuunda serikali ya umoja, kurekebisha katiba, kufanya uchaguzi mkuu mpya na kupambana na ugaidi.

  Habari nyingine zinasema China imesaini makubaliano ya kutoa misaada ya kiuchumi, kiufundi na chakula kwa Syria ili kuisaidia kukabiliana na hali ngumu ya sasa, ikiwa ni hatua ya kutekeleza ahadi iliyotoa China kwenye mkutano wa Baraza la Ukanda mmoja na Njia moja uliofungwa jana hapa Beijing.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako