• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yapata uungaji mkono wa AU katika kukomesha mapambano Darfur

    (GMT+08:00) 2017-05-16 10:04:26

    Serikali ya Sudan imesema Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika AUPSC limesisitiza uungaji mkono wake kwa juhudi zilizofanywa na Sudan katika kukomesha mapambano kwenye eneo la Darfur.

    Ahadi hiyo imetolewa baada ya ziara ya siku nne ya ujumbe wa baraza hilo nchini Sudan. Taarifa iliyotolewa na Wizara ya mambo ya nje ya Sudan imesema ujumbe huo umepongeza maendeleo yaliyopatikana Darfur na kwenye ushirikiano kati ya serikali ya Sudan na baraza hilo. Umoja wa Afrika pia utaiunga mkono Sudan katika juhudi zake za kutatua masuala ya Afrika kwa njia za kiafrika.

    Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Sudan Bw Aristide Nononsi, amesema Sudan imepata maendeleo makubwa katika mambo ya haki za binadamu, na kwamba yuko tayari kuipatia Sudan misaada ya kiufundi kwenye eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako