• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yatuma wataalamu wa matibabu katika mikoa inayopakana na DRC ili kudhibiti Ebola

    (GMT+08:00) 2017-05-16 10:15:34

    Tanzania imetuma timu ya wataalamu wa matibabu katika mikoa sita ili kuboresha mfumo wa utambuzi na mawasiliano kuhusu mlipuko wa homa ya Ebola.

    Hatua hiyo imechukuliwa siku tatu baada ya Shirika la Afya Duniani WHO kutangaza mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.

    Katibu mkuu wa wizara ya afya, maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto Bw. Mpoki Ulisubisya amesema wataalamu hao wametumwa kwenye mikoa ya Mwanza, Kagera, Kigoma, Katavi, Rukwa na Songwe. Ameongeza kuwa wamechagua mikoa hiyo kutokana na kuwa inakabiliwa na tishio kubwa, kwa kuwa watu wanaodhaniwa kuambukizwa virusi vya Ebola wanaweza kujipenyeza kupitia mikoa hiyo kama hatua hazijachukuliwa.

    Serikali ya Zambia pia imeimarisha usimamizi katika maeneo yanayopakana na DRC kufuatia mlipuko wa Ebola.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako