• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lalaani mashambulizi dhidi ya askari wake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

    (GMT+08:00) 2017-05-16 16:40:02

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali mashambulizi yaliyofanywa hivi karibuni na wapiganaji wa kundi la anti-balaka dhidi ya kikosi cha kulinda amani wa Umoja huo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA, raia, na wahudumu wa kibinadamu nchini humo.

    Taarifa iliyotolewa na Baraza la Usalama imesema mashambulizi hayo yamesababisha kuuawa kwa askari mmoja wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Morocco, na askari mmoja kutoka Morocco na raia kadhaa kujeruhiwa, na watu wengi kukimbia makazi yao.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameaani vikali mashambulizi hayo na kuzitaka mamlaka husika kufanya uchunguzi na kuwafikisha watuhumiwa kwenye vyombo vya sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako