• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yasema pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja ni mfano bora wa ukuaji barani Afrika

    (GMT+08:00) 2017-05-16 16:40:28

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema kuwa pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja ni mfano mzuri wa mchakato wa maendeleo barani Afrika.

    Rais Kenyatta amesema hayo katika mkutano wa meza ya duara wa viongozi uliofanyika jana hapa Beijing. Amesema bara la Afrika liko tayari kuchukua tena fursa ilizokosa za utandawazi kwa kuchukua nafasi muhimu katika pendekezo hilo la China kwa ajili ya mwingiliano wa dunia.

    Wakati huohuo, mtafiti kutoka Kituo cha Elimu ya Usalama kilichopo Addis Ababa, Ethiopia, Ndubuisi Christian Ani amesema, pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja lililotolewa na China ni msaada mkubwa kwa kupanua ushirikiano wa kimataifa na maendeleo. Amesema pendekezo hilo liko sambamba na hitaji kubwa la Afrika la maendeleo ya miundombinu na uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako