Uchunguzi uliofanywa na Shirika la Watumizi wa Bidhaa Kenya (Cofek) umebaini kuwa wakenya karibu milioni 20 hawapati kiamsha kinywa kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.
Uchunguzi huo umebaini kuwa wakenya wengi hawanywi tena chai wala uji asubuhi kutokana na kupanda kwa bei ya unga,maziwa na sukari.
Katibu Mkuu wa Cofek Stephen Mutoro amesema migahawa na hata vibanda vya kuuzia chai sasa vimepandisha bei ya vyakula.
Bw Mutoro amesema wateja wameathiriwa zaidi kwa sababu hata vibanda vya chakula vimeongeza bei kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu.
Hivi sasa pakiti ya maziwa inauzwa kwa Sh70 ,huku mfuko wa unga wa mahindi ukiuzwa kwa Sh180.
Uchunguzi uliofanywa na Cofek unaonyesha kuwa wakenya wengi walisema wamelazimika kukwepa kiamsha kinywa kwa sababu hiyo ndio njia pekee ya kukwepa kutumia pesa nyingi kununua maziwa na sukari.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |