• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda-IMF yakadiria uchumi wa Rwanda kukua kwa 6.2% mwaka 2017

    (GMT+08:00) 2017-05-16 19:34:44

    Shirika la Fedha Duniani (IMF) limekadiria kuwa uchumi wa Rwanda utakua kwa asilimia 6.2 mwaka 2017,tofauti na mwaka 2016 ambapo uchumi ulikua kwa asilimia 5.9.

    IMF inakadiria kuwa ukuaji wa uchumi utaongezeka zaidi mwaka huu kutokana na kufufuka kwa sekta ya kilimo,ukuaji wa mauzo ya nje,na kupungua kwa nakisi ya biashara.

    Shirika hilo linasema kuwa juhudi za serikali na motisha ya kuimarisha uzalishaji wa ndani na matumizi ya bidhaa za ndani utaimarisha uchumi.

    Mkuu wa IMF Laura Redifer amesema ukuaji wa uchumi unatarajiwa kuboreka mwaka huu kutokana na mvua zinazoshuhudiwa na pia kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa ndani.

    Kulingana na takwimu zilizotolewa na Benki Kuu ya Rwanda mwezi Januari ,nakisi ya biashara ilishuka kutoka $1,602.21 million hadi $1,519.97 million katika miezi 11 ya kwanza ya mwaka 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako