• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania yanufaika na Miradi ya ujenzi wa miundo mbinu

  (GMT+08:00) 2017-05-17 00:14:10
  Mkutano wa baraza la ukanda mmoja njia moja ulifungwa jana hapa Beijing. Muda mfupi baada ya kufungwa kwa mkutano huo, viongozi mbalimbali walioshiriki kwenye mkutano huo, wamekuwa wakieleza ni nini kimejadiliwa kwenye mkutano huo, na vipi nchi zao zimejipanga kunufaika na fursa zinazoletwa na mkutano huo. Mwenzetu Fadhili Mpunji amepata fursa ya kuongea na waziri wa ujenzi, mawasiliano na uchukuzi wa Tanzania Profesa Makame Mbarawa aliyemwakilisha Rais wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli, na kutuandalia ripoti ifuatayo.

  Tanzania ni moja ya nchi ambazo ni wadau wa pendekezo la mpango wa "ukanda mmoja, njia mmoja", na tayari imeanza kunufaika na miradi ya pendekezo la ukanda mmoja na njia moja. Baadhi ya miradi ya pendekezo hilo imeanza kutekelezwa, na miradi mingine iko mbioni kutekelezwa. Lakini kwanza Waziri Mbarawa anafahamisha: "Kuanzia tarehe 14 mpaka tarehe 15 Mei kulikuwa na mkutano mkuu wa Kimataifa ambao unaitwa mkutano wa "ukanda mmoja, Njia moja" , ambao unakusanya wanachama wa mkutano huo ambao Tanzania moja wa umoja huu, ambao kazi yake ni kuangalia jinsi ya kuunganisha maeneo yote hayo katika Ukanda mmoja unaofanya usafirishaji uwe rahisi, ili kuhakikisha uchumi wa nchi zetu unakuwa pamoja na unakua kasi inayotakiwa. Kwa vile mimi kama waziri wa sekta yote ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano ninapata fursa ya kumwakilisha rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli, na katika mkutano huo mimi nilipata heshima nyingine ya kuweza kuzungumza kwenye mkutano ule jinsi gani Tanzania tumejipanga mpango huo, na jinsi gani Tanzania tunaweza kufaidika kwenye mkutano huo. Bahati nzuri walikuwa wenzangu kutoka nchi mbalimbali lakini nilipata fursa nikiongelea maeneo mbalimbali ambayo Tanzania tunafikiria kwamba tukishirikiana na wenzetu hasa China kwa sababu ni kiongozi kwenye mkutano huu tukaweza kunufaika kwanza.

  Eneo la kwanza kabisa ni ujenzi wa reli ya Kati ambayo serikali ya Tanzania imeanza kumpa kandarasi kwa awamu ya kwanza ambao ni kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro na tunatumia pesa zetu za ndani na tumekidha pale kama 1.2 bilioni kwa ajili ya ujenzi huo, na treni hiyo itakuwa treni ya kisasa ambayo itakuwa treni ya kutumia umeme na pia ni treni yenye mwendo kasi wa kilomita 160 kwa saa, treni hii itakapokamilika itaweza kubadilisha kabisa utaratibu wote wa usafirishaji hasa kanda ya kati. Mradi huu mwenyewe utaunganisha nchi mbalimbali za jirani kwa mfano Burundi, Rwanda, Uganda…Pia serikali ya Tanzania imeamua kipaumbele chetu kimoja ili kuhakikisha usafirishaji wa anga unaimarika na kufufua upya shirika la ndege la Tanzania, ili kufanya usafiri wa anga utakua ili kuchangia katika uchumi wa nchi yetu."

  Kama alivyoeleza Profesa Mbarawa, moja ya malengo ya pendekezo la ukanda mmoja, na njia moja sio tu ni kuunganisha China na nchi zilizoko kwenye eneo la ukanda huo, bali pia ni kuzifanya nchi zilizoko kwenye ukanda huo ziungane zenyewe kwa zenyewe na kuwanufaisha wananchi wao.

  Moja ya taarifa iliyopatikana baada ya mkutano huo ni kuwa serikali ya Tanzania inafanya juhudi kuhakikisha kuwa, Tanzania inanufaika na soko la utalii la China, na sasa inafanya maandalizi ya kuwa na safari za ndege za moja kwa moja kati ya Tanzania na China.

  Leo pia waziri Mbarawa ameshuhudia kusainiwa kwa makubaliano ya kuingiza bidhaa za muhogo kwenye soko la China, yaliyoswaniwa kati ya Balozi wa Tanzani Mh Mbelwa Kairuki, na naibu mkuu wa idara ya usamizi wa ubora, ukaguzi na karantini ya China Bw Li Yuanping.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako