• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashindano ya Riadha Afrika Mashariki kwa vijana U-17

    (GMT+08:00) 2017-05-17 08:44:42
    Mashindano ya riadha kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 yamefunguliwa jana jijini Dar es salaam na Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo wa Tanzania Dr. Harrison Mwakyembe na kueleza kuwa mchezo wa riadha umekuwa na mchango mkubwa katika kukuza na kuimarisha ushirikiano baina ya Afrika mashariki na kati.

    Katika mashindano hayo, jana Kenya waliibuka kidedea kwa kuzoa medali 3 za dhahabu kwenye mbio za mita 800 kwa wasichana na wavulana pamoja na mita 3000, huku Tanzania ikiibuka kidedea katika mita 100 kwa wasichana katika mchezo wa kubadilishana vijiti.

    Mashindano hayo ya siku mbili yanakamilika leo yanahusisha timu 7 za Afrika mashariki na kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako